Ubongo Kids Kiswahili

Nyimbo mbili "Mwanga na ala za muziki!" | imba na Ubongo Kids | Katuni za Kiswahili

Ubongo Kids inamjenga mwanao, ikimpa fikra komavu zitakazomwezesha kutambua kusudi lake masomoni na maishani! Njoo nasi Kokotoa, ukajifunze kutumia uwezo na utashi wako kusuluhisha changamoto zinazokukabili ili ufike pale utakapo! Ubongo Kids ni mfululizo wa hadithi za kusisimua zilizo katika mfumo wa elimu-burudani kwa ajili ya watoto wa miaka 7 hadi 13, zikitumia nyimbo na maudhui ya Kiafrika kuwafundisha hisabati na sayansi! Katuni hii mahususi ya elimu inaandaliwa na Ubongo Learning, ambao pia ni watengenezaji wa kipindi murua ya Akili and Me inayowaandaa watoto wa miaka 3-6 kwa ajili ya kwenda shule! Tazama Ubongo Kids kila Jumamosi na Jumapili saa 3 asubuhi kupitia TBC1! Pata pia webisodes zetu zote kupitia: https://www.ubongokids.com https://www.facebook.com/ubongokids/ Created by Ubongo, the Tanzanian social enterprise that entertains kids to learn and love learning! https://www.ubongo.org Made possible by the Human Development Innovation Fund, funded by UKAid.

Sep 24, 2020